Story by Correspondents –
Serikali imeongeza mda wa wiki mbili kwa wanafunzi wa darasa la nane na kidato cha nne kote nchini kusajiliwa katika mtihani wa kitaifa wa KCPE na KCSE wa mwaka wa 2021.
Waziri wa Elimu nchini Prof, George Magoha amesema usajili huo umeongezewa mda hadi tarehe 14 mwezi huu wa Agosti ili kuhakikisha shule zinawasajili wanafunzi wote watakaokalia mtihani huo.
Waziri Magoha amesema serikali imeafikia uamuzi huo baada ya walimu wakuu na wasimamizi wa shule hizo kuomba kuongezewa mda zaidi licha ya usajili huo kuhitaji kukamilika mwezi Julai, 31.
Waziri Magoha amedokeza kuwa wanafunzi watakaokosa kusajiliwa katika mtihani huo utakaoandaliwa mwezi Machi mwaka wa 2022, basi watalazimika kukalia mtihani huo mwezi Disemba mwaka huo wa 2022 wakati Wizara ya elimu itakapoandaa mtihani mwengine.
Wakati uo huo Wakurungezi wa elimu katika kaunti mbalimbali nchini wameagizwa kutuma sajili ya vituo vitakavyotumika kuandaa mtihani huo wa kitaifa kabla ya tarehe 10 mwezi Septemba mwaka huu.