Picka kwa hisani –
Huku shughuli za masomo zikiingia siku ya pili hii leo wanaharakati wa masuala ya kijamii katika kaunti ya Kwale wamesema serikali imejizatiti kuboresha miundo msingi ya shule ili kuthibiti maambukizi ya corona.
Wakiongozwa na Mohamed Mwachausa wa shirika la Samba Sports Youth Agenda,wanaharakati hao wamesema serikali imeweka juhudi kuhakikisha shule za humu nchini zinapata vifaa vya kuwakinga wanafunzi na maambukizi.
Wanaharakati hao aidha wamesema kuna haja ya serikali,wazazi na wasimamizi wa shule kukaa chini kujadili jinsi ya kutatua changamoto zitakazo jitokeza miongoni mwa wanafunzi kipindi hiki cha janga la corona.