Picha Kwa Hisani –
Serikali imeanzisha utafiti kuhusu rasilimali ya samaki katika Bahari hindi ili kupanua sekta ya uvuvi nchini.
Waziri wa kilimo, mifugo, uvuvi na vyama vya akiba na mikopo Peter Munya amesema hatua hiyo imeafikiwa ili kuiweka Kenya kileleni katika maswala ya uvuvi na kuimarisha uchumi wa baharini.
Akizungumza huko Shimoni alipokutana na wadau katika sekta ya uvuvi, Munya amesema kituo maalum kitaidhinishwa katika eneo hilo ili kutoa mafunzo kwa wavuvi na wataalam wengine katika kuboresha uchumi wa baharini.
Munya amesema kituo hicho maalum kitatoa nafasi kwa wenyeji kuwekeza katika shughuli za uvuvi ili mbali na kujiinua kimapato na Serikali inufaike na raslimali katika Bahari hindi.