Story by Gabriel Mwaganjoni:
Serikali itatekeleza ujenzi wa madarasa katika shule mbalimbali za umma kote nchini sawia na ukanda wa Pwani ili kuwakimu wanafunzi watakaokuwa wakiingia kidato cha kwanza baada ya kufikia darasa la sita.
Mshirikishi mkuu wa utawala kanda ya Pwani John Elungata amesema mpango huo tayari umeanza kutekelezwa kwani wanafunzi hao wanapaswa kuanza masomo yao ya upili chini ya mfumo mpya wa 2-6-6-3 mwakani.
Elungata amesema mpango huo unatekelezwa na Serikali ya kitaifa.
Wakati uo huo, amewataka mafundi na wataalam wengine wa ujenzi kupewa nafasi za ujenzi wa madarasa au miradi mingine yoyote ya upanuzi wa shule na wala sio kwa makamishna wa kaunti kuwatafuta mafundi kutoka maeneo tofauti.