Picha kwa hisani –
Serikali ya kaunti ya Kwale, sasa inaitka serikali ya kitaifa kupitia Wizara ya Madini nchini kuhakikisha mgao wa fedha unaotokana na raslimali za madini katika kaunti hiyo zinasambazwa kwa serikali ya kaunti hiyo.
Naibu Gavana wa Kwale Bi Fatuma Achani amesema serikali ya kaunti hiyo haijafaidika na fedha hizo za uchimbaji wa madini unaoendelezwa na kampuni ya Base Titanium katika eneo la Msambweni.
Kiongozi huyo amedai kushangazwa na hatua ya serikali ya kitaifa ya kukosa kusambaza fedha hizo kwa serikali ya Kwale kwa mda mrefu licha ya mgao huu kupatikana katika maeneo ya kaunti ya Kwale.
Achani amesema kulingana na taratibu za mgao wa fedha hizo, serikali ya kaunti ya Kwale inafaa kupokea mgao wa asimilia 30 ambapo asimilia 10 inafaa kugawa kwa jamii za eneo hilo.