Picha kwa hisani –
Seneta wa Kaunti ya Baringo Gideon Moi amewalaumu baadhi ya mahasimu wake wa kisiasa katika eneo la Bonde la Ufa kwa kumdhalilisha kisiasa kwenye ziara yake katika Kaunti ya Nandi.
Kwenye tukio la siku ya Jumamosi vijana waliokuwa wamejawa na ghadhabu kutoka Kaunti ya Nandi walimzuia Senata Moi dhidi ya kuingia katika Kaunti hiyo.
Seneta huyo ambaye pia ni kiongozi wa Chama cha Kanu alikuwa akielekea katika Kaunti ya Nandi kufanya mkutano na naibu mwenyekiti wa baraza la Wazee wa Talai Christopher Koyogi.
Aidha vijana hao wanaodaiwa kumuunga mkono naibu rais William Ruto wamemlaumu Gideon kwa kwenda kinyume na tamaduni za baraza hilo la wazee kwani lilikuwa tayari limemtangaza naibu Rais kuwa Kiongozi wa eneo hilo.
Hata hivyo Moi amelaani tukio hilo la kumdhalilishwa na kusema kuwa halitarudisha nyuma azma yake ya kuendeleza siasa zake kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2022.