Picha kwa hisani –
Viongozi mbali mbali nchini wametuma rambi rambi zao kwa familia ya aliyekua waziri wa ulinzi nchini seneta wa Garissa Yusuf Hajji aliyeaga dunia asubui ya leo katika hospitali ya Aga Khan Nairobi akiwa na miaka 80.
Rais Uhuru Kenyatta amemtaja mwendazake Hajj,ambae pia ni babake mkurugenzi wa mashtaka ya umma nchini Noordin Hajj,kama kiongozi mwenye busara na aliyekua nguzo muhimu ya kujenga mshikamano,amani na maendeleo ya taifa.
Kwa upande wake naibu wa rais William Ruto na mwenzake kinara wa ODM Raila Odinga wamemtaja marehemu Hajj,kama kiongozi myenyekevu aliyejitolea kulihudumia taifa na aliyekua na uwezo mkubwa wa kusuluhisha mivutano.
Maseneta wakiongoza na spika wa bunge la seneti Keneth Lusaka wamemtaja mwendazake Hajj kama seneta aliyesaidia pakubwa katika kusuluhisha mizozo iliyoibuka kati ya maseneta wakati wa kujadili miswada mbali mbali bungeni.
Mwanasiasa huyo mkongwe alihudumu kama waziri wa ulinzi kati ya mwaka 2008 – 2013 na akahudumu kwa muda mfupi kama kaimu waziri wa usalama wa ndani na masuala ya kigeni mwaka 2012 na amehudumu kama seneta wa Garissa tangu mwaka 2013 hadi kifo chake,na atazikwa alasiri ya leo katika maziara ya Langata Nairobi.