Picha kwa hisani –
Seneta wa Kilifi Stewart Madzayo amewasuta baadhi ya maafisa wakuu wa serikali ya kaunti ya Kilifi kwa madai kwamba wamewapuuza vijana wanaotafuta ajira katika idara mbali mbali za serikali ya kaunti hiyo.
Madzayo amesema vijana wengi waliohitimu na ambao wanaweza kuajiriwa kwenye idara mbali mbali wamesalia kuhangaika mitaani huku mkuu wa kitengo cha utoaji zabuni akitoa zabuni kiubaguzi
Madzayo aidha amemtaka gavana wa Kilifi Amason Jeffa Kingi kutokubali maafisa wachache wa kaunti hio kuendeleza utepetevu na badala yake kuwachukulia hatua kali.