Seneta wa Mombasa Mohammed Faki amesema kuwa hali ya vijana wenye umri mdogo katika eneo la Kisauni kujihusisha na uhalifu itamalizika, vijana hao wakisaidiwa kuimarisha vipaji vyao hasa katika kandanda.
Akiongea wakati wa uzinduzi wa mchuano wa Ahmed Mohammed Chucho memorial Cup eneo la Junda huko Kisauni Faki amehoji kwamba vijana wengi wamejiingiza katika uhalifu na utumizi wa mihadarati kwa kukosa uungwaji mkono katika kukuza talanta zao.
Faki amesema kuwa kupitia kwa michuano ya michezo mbali mbali vijana wengi watasaidiwa kujitenga na ushawishi wa makundi ya kihalifu.
Taarifa Na Hussein Mdune