Seneta wa Kaunti ya Mombasa Mohammed Faki amependekeza kufunguliwa kwa nyumba za Ibada nchini na hasa misikiti ili kutoa nafasi kwa waumini wa dini ya Kiislamu kuendeleza ibada zao wakati wa Mwezi mtukufu wa Ramadhan.
Akiwahutubia wanahabari Mjini Mombasa Faki amesema hali itakuwa tata zaidi kwa waumini wa dini ya Kiislamu endapo misikiti haitafunguliwa kadri mwezi mtukufu wa Ramadhan unapowadia.
Faki amesema katika mswada maalum unaofungamana na maswala ya ugonjwa wa Corona katika bunge la Seneti watapendekeza maswala hayo ya kidini yajumuishwe kwenye mswada huo.
Aidha ameitaka Serikali kupunguza ushuru kwa bidhaa msingi za matumizi ya kila siku ili kumuondolea mwananchi wa chini gharama ya maisha.
Wakati uo huo, ameitaka Serikali kuijumuisha misikiti katika mradi wake wa ugavi wa chakula cha msaada kwa wale wasiyobahatika katika jamii.