Picha kwa hisani –
Kiranja wa walio wengi katika bunge la Seneti Irungu Kang’ata amejitokeza na kutetea kauli yake aliyoitoa kuwa mchakato wa kuifanyia marekebisho Katiba kupitia BBI hauna umaarufu katika eneo la Mlima Kenya.
Kang’ata amesema barua aliyomuandikia rais Uhuru Kenyatta kuhusiana na takwimu za BBI katika eneo la Mlima Kenya, ni ukweli mtupu na kuna haja ya kiongozi wa taifa kuichukulia kwa uzito barua hiyo.
Kang’ata ambaye pia ni Seneta wa kaunti ya Murang’a, amesema yuko tayari kwa hatua yoyote ambayo wakenya ama Rais Kenyatta atamchukulia huku akihoji kuwa ni lazima ukweli kuhusiana na mchakato wa BBI katika eneo la Mlima Kenya usemwe.
Wakati uo huo amesema ni lazima kwa viongozi wanaopendekeza kupitishwa kwa BBI kuibuka na mikakati tofauti itakayochangia wakenya kuunga mkono BBI kwani jinsi hali ilivyo mashinani huenda BBI ikakosa kupata umaarufu.