Seneta maalum wa chama cha Jubilee Christine Zawadi amelaani vikali hatua ya kutimuliwa kwa Mbunge wa Malindi Aisha Jumwa kutoka kwa chama cha ODM.
Aisha alitimuliwa kutoka ODM kwa madai ya kuasi chama.
Zawadi amesema hatua hiyo imedhihirisha wazi kuwa uongozi wa chama cha ODM ni wakidikteta na hauna nia ya kuleta uwiano licha ya kuwa Aisha amekuwa msitari wa mbele katika kutetea maslahi ya chama.
Hata hivyo amewataka viongozi wenzake wa Pwani kuendelea kushirikiana na viongozi wa jinsia ya kike katika harakati za kuendeleza maendeleo kwa jamii.
Taarifa na Marietta Anzazi.