Story by Gabriel Mwaganjoni –
Licha ya sekta ya uchukuzi wa umma ya Bodaboda kuwa na umuhimu mkubwa kiuchumi katika kaunti yoyote ile, sekta hiyo imetelekezwa mno.
Kulingana na Mwanasiasa Mhandisi Mkalla Chitavi, sekta hiyo hasa katika kaunti ya Mombasa haijapewa nafasi wala idara ya trafiki, ile ya uchukuzi katika kaunti ya Mombasa na washirika wengine wa kibiashara hawajajadili muelekeo unaofaa kuchukuliwa ili kuwastawisha wanabodaboda.
Akizungumza katika eneo la Tononoka kaunti ya Mombasa alipokutana na wahudumu wa Bodaboda, Chitavi amekariri kwamba sekta hiyo inapaswa kutambuliwa na kukuzwa ili wahudumu katika sekta hiyo waimarike kibiashara.
Wakati uo huo, amezitaka taasisi za kifedha na mikopo kushusha riba kwa viwango vya mikopo wanavyotoa kwa wanabodaboda akisema riba hizo za juu zimepelekea wanabodaboda kushindwa kujiendeleza kibiashara.