Serikali ya kaunti ya Kwale imenufaika na mashini mpya, itakayotumika katika matibabu ya ugonjwa wa saratani ya kizazi.
Akizungumza baada ya kumkabidhi muuguzi mkuu wa kaunti ya Kwale Edward Mumbo mashini hiyo kwa jina Cryotherapy, afisa kutoka kampuni ya Base Titanium Pius Kassim amesema mashini hiyo yenye thamani ya shilingi nusu milioni, itawawezesha madaktari kufanya upasuaji maalum wakitumia mbinu mpya za kitaalam.
Aidha Kassim amedokeza kuwa jumla ya wauguzi 28 wameanza kupokea mafunzo maalum kuhusu jinsi wanavyoweza kuitumia mashini hiyo katika matibabu ya saratani ya kizazi.
Taarifa na Gabriel Mwaganjoni.