Mwanamke mmoja wa umri wa makamo hii leo amepata majeraha baada ya bodaboda ambayo alikuwa ameabiri kugongana na gari dogo katika barabara ya Kombani Kwale sehemu ya Kwale mjini.
Kulingana na OCS wa kituo cha polisi mjini Kwale Ludwin Sasati gari nambari ya usajili KCB 599 R lililokuwa likiendeshwa na Ali Mukumi liligongana na bodaboda ambayo ilikuwa ikiendeshwa na Juma Zuma kwa mwendo wa kasi.
Abiria kwa jina Mwanaiki Bakar Siri ambaye alikuwa kwenye pikipiki ya Juma Zuma alianguka chini na kupata majera kichwani na kisha akakimbizwa katika hospitali ya Kwale kwa matibabu na akaruhusiwa kwenda nyumbani.
Aidha Sasati amewataka madereva na waendeshaji boda boda kuzingatia sheria za trafiki wakati wanapokuwa barabarani .