Mahakama ya mjini Kwale imepokea sanduku maalum kutoka kwa shirika la kukabiliana na dhulma dhidi ya watoto la Haki Yetu litakalotumiwa na watoto wanaodhulumiwa kutoa ushahidi.
Akiongea wakati wa kupeana sanduku hilo afisa wa mipango kutoka shirika hilo Munira Aboubakar amesema mara nyingi kesi za dhulma za kijinsia dhidi ya watoto husambaratika kutokana na hatua ya watoto kuogopa kutoa ushahidi wao.
Abubakar ameitaka jamii kuwaandaa watoto kisaikolojia kabla ya kufikishwa mahakamani sawa na kuwashauri kutoogopa kutoa ushahidi.
Kwa upande wake mkurugenzi wa masuala ya watoto kaunti ya Kwale Stephen Gitao amepongeza kuwasilishwa kwa sanduku hilo akisema kuwa kutaimarisha vita dhidi ya dhulma za kijinsia kwa watoto.
Taarifa na Mariam Gao.