Story by Gabriel Mwaganjoni –
Gavana wa kaunti ya Taita Taveta Granton Samboja amesema amejizatiti katika kuboresha sekta ya afya katika kaunti hiyo.
Samboja amesema ikilinganishwa na hali ilivyokuwa hapo awali, sekta ya afya katika kaunti hiyo inafanya vyema huku wakaazi waliyolazimika kusafiri katika kaunti nyingine kutafuta matibabu maalum wanatibiwa katika hospitali kuu ya rufaa ya Moi mjini Voi.
Samboja amesema licha ya changamoto nyingi zinazoikumba Serikali ya kaunti hiyo hasa kuhusu uchache wa fedha sekta ya afya katika kaunti Taita taveta imeimarika pakubwa.
Wakati uo huo Samboja amewakosoa wale wanaotumia kipengele cha afya kujipigia debe katika uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2022 akisema hawana agenda yoyote ya maendeleo.