Story by Our Correspondents –
Gavana wa kaunti ya Taita taveta Granton Samboja amezindua mradi wa maji wa Di Moody nakuruto, katika eneo la Taveta katika kaunti hiyo ambao utawanufaisha zaidi ya wakaazi elfu 17 kutoka wadi za Mwaghogho na Chala.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mardi huo, Samboja amesema mradi huo ni suluhu la tatizo la uhaba wa maji ambalo limekuwa likiwakabili wakaazi kwa mda mrefu.
Samboja hata hivyo ameiagiza Wizara ya maji katika serikali ya kaunti hiyo kuwaunganishia wakaazi hao maji bila malipo na wakaazi hao wapewe mda wa kulipa ada za mita za maji kwa awamu.