Baada ya usimamizi wa kiwanda cha maziwa cha Brookside kusitisha ununuzi wa maziwa kutokwa kwa wafugaji katika Kaunti ya Taita taveta, sasa Gavana wa Kaunti hiyo Granton Samboja ameingilia kati utata huo.
Kulingana na Samboja kiwanda hicho kimekuwa kikipata lita 2,000 za maziwa badala ya kiwango cha hapo awali cha lita 5,500 hali iliyousukuma usimamizi wa kiwanda hicho kufunga biashara yake Kaunti hiyo.
Samboja amewakosoa wafugaji katika Kaunti hiyo kwa kuingiza siasa katika mchakato huo wa biashara ya maziwa hasa baada ya kuhadaiwa na madalali katika Kaunti hiyo.
Wakati uo huo, Samboja amewatahadharisha wafugaji hao dhidi ya kuhadaiwa na madalali katika eneo hilo hali ambayo imedidimiza kabisa biashara hiyo ya maziwa na kuwanyima pato wafugaji hao sawa na Kaunti hiyo.