Gavana wa kaunti ya Taita Taveta Granton Samboja amebanduliwa mamlakani na wawakilishi wadi wa kaunti hio.
Hii ni baada ya wawakilishiwadi 30 katika kaunti hio kuunga mkono hoja ya kumbandua mamlakani samboja iliowasilishwa na kiongozi wa waliowengi katika bunge hilo Harris Keke.
Awali wajumbe katika bunge la kaunti ya Taita Taveta walimkashifu gavana samboja kwa matumizi mabaya ya afisi hasa baada ya kushuhudiwa mgogoro kati yao kuhusu utekelezwaji wa bajeti ya mwaka wa kifedha 2019/2020.
Viongozi mbali mbali humu nchini waliingilia kati kuusuhisha mgogoro huo,juhudi ambazo hazikuzaa matunda.