Story by Ali Chete-
Naibu mkurugenzi wa Shirika la kutetea haki za kibinadamu la Haki Africa Salma Hemed amesema ukosefu wa ajira miongoni mwa vijana ndio chanzo cha vijana wengi katika ukanda wa Pwani kujiunga na makundi ya kihalifu.
Akizungumza katika kaunti ya Mombasa, Salma amesema takwimu zimeonyesha idadi kubwa ya vijana wamejiunga na makundi ya itikadi kali, kwa kisingizo cha ukosefu wa ajira.
Mwanaharakati huyo wa kijamii amesema kuna haja ya serikali kuwekeza zaidi katika swala la ajira badala ya kuwaacha vijana wengi wakirandaranda ovyo mitaani.