Story by Gabriel Mwaganjoni –
Takwimu zilizotolewa na wakereketwa wa maswala ya jinsia na haki za watoto kanda ya Pwani, zimeonesha wazi kwamba zaidi ya watoto elfu moja walidhulumiwa kingono na wengine kupachikwa mimba mwaka wa 2020.
Naibu mkurugenzi wa Shirika la utetezi wa haki za kibinadamu la Haki Afrika Salma Hemed amesema takwimu hizo zinasikitisha huku akipendekeza kila mbinu kuidhinishwa ili kuikabili hali hiyo.
Akizungumza katika kaunti ya Mombasa, Salma amesema ni sharti Serikali iwekeze zaidi katika kumlinda mtoto ambaye kwa sasa yuko hatarini.
Wakati uo huo, amedokeza kuwa japo juhudi zaidi zimeidhinishwa ili kuangazia maslahi ya mtoto katika ukanda wa Pwani bado mbinu zaidi zinahitajika kuekezwa.