Story by Taalia Kwekwe-
Afisa miradi katika shirika la kijamii la The Hijabi Mentorship Salama Majaliwa amesema wameanzisha miradi mbali mbali ikiwemo ule wa Nikumbuke Soccer kama njia mojawapo ya kuwezesha wanawake mashinani.
Kulingana na Salama, mradi huo ambao umefadhiliwa na The US Embassy unalenga akina mama na wasichana wanaopitia changamoto ikiwemo dhulma za kijinsia na sharti wawe wa umri wa miaka 22 kuendelea.
Wakati uo huo Salama amesema kupitia mradi huo wa kandada wanawake wamefaidika kwa mambo mengi ikiwemo kudhibiti msongo wa mawazo.