Story by Bakari Ali –
Kampuni ya mawasiliano humu nchini Safaricom ikishirikiana na benki ya Gulf African imezindua mtandao unaolenga kutoa mikopo kupitia simu za rununu maarufu Halal Pesa chini ya usimamizi na taratibu za kiislamu yaani Shari’ah law.
Mkurugenzi mkuu wa kampuni hiyo Peter Ndegwa amesema mtandao huo unanuia kushirikisha jamii na dini mbalimbali nchini katika masuala ya kibiashara.
Ndegwa amesema mtandao huo utatumika kitaifa licha ya lengo kuu ya mtandao huo ni kulenga jamii ya kiislamu nchini.
Kwa upande wake mkurugenzi mkuu wa benki ya Gulf African Abdallah Abdulhalik amepongeza ushirikiano huo baina ya kampuni ya Safaricom na benki hiyo, akisema uzinduzi wa mtandao huo unaolenga kuunganisha jamii mbalimbali kibiashara na maendeleo.