Kampuni ya mawasiliano ya Safaricom imemteua Peter Ndegwa kama afisaa mkuu mtendaji.
Ndegwa ambaye amewahi kuwa mkurugenzi wa fedha katika kampuni ya vileo ya East African Breweries ataingia madarakani Aprili 1 mwaka wa 2020.
Bwana Ndegwa anakuwa mkenya wa kwanza kuongoza kampuni hiyo ya mawasiliano ambayo kwa sasa inaongozwa na Michael Joseph baada ya kufariki kwa Bob Collymore.