Story by Mimuh Mohamed –
Mwakilishi wa kike katika kaunti ya Murang’a Sabina Chege amefika mbele ya kamati ya nidhamu ya tume huru ya uchaguzi na mipaka nchini IEBC kuhojiwa kuhusiana na matamshi ya wizi wa kura anayodaiwa kuyatoa wakati wa mkutano wa mkutano wa hadhara katika eneo la Vihiga.
Wakati wa kikao hicho mawakili wa Sabina wakiongozwa na Otiende Amollo, James Orengo na Martin Oloo, wameibua maswali kuhusu iwapo IEBC ina uwezo wa kisheria kuchunguza suala hilo ikizingatiwa kwamba sio kipindi rasmi cha kampeni.
Imewalazimu makamishana wa kamati ya nidhamu ya tume ya IEBC chini ya Mwenyekiti wake Wafula Chebukati kuchukua dakika kadhaa kujadiliana katika kikao cha faragha kuhusu iwapo tume hio ina uwezo wa kuendelea na kesi hiyo.
Chebukati hata hivyo amepuuzilia mbali hoja iliyoibuliwa na mawakili hao na kuweka wazi kwamba IEBC itaendelea kusikiliza kesi hiyo kwa kuambatana na sheria ya uchaguzi.
Katibu wa kamati ya nidhamu ya IEBC amepata fursa ya kusoma mashtaka yanayomkabili Sabina sawa na kunukuu matamshi aliyotamka kiongozi huyo.