Picha kwa hisani –
Naibu wa rais Dkt William Ruto amewataka wanasiasa wanaomezea mate wadhfa wa urais kwenye uchaguzi mkuu ujao kujitafutia kura kwa wananchi badala ya kusubiri kupigiwa debe na rais Uhuru Kenyatta.
Akihutubia wakaazi wa eneo bunge la Kinango wakati wa ziara yake ya siku tatu katika eneo la Pwani, Ruto amesema rais Kenyatta hawezi kuwaunga mkono wanasiasa waliokua mahasimu wake hapo awali.
Wakati uo huo, amewataka vijana kutokubali kutumiwa vibaya na wanasiasa na badala yake kuunga mkono vugu vugu la hustlers lenye nia ya kuwainua kiuchumi walala hoi.
Kwa upande wake Mbunge wa Kinango Benjamin Dalu Tayari ameapa kuendeleza kampeni za kumpigia debe Ruto katika eneo hilo ili kuhakikisha wakaazi wanamuunga mkono kwenye uchaguzi ujao.