Story by Our Correspondents-
Rais William Ruto ameahidi kuhakikisha kila mmoja anawajibikia majukumu yake ya kikazi katika kila sehemu anapofanya kazi ili kuhakikisha taifa hili linasonga mbele kimaendeleo na kuimarika kiuchumi.
Kiongozi wa taifa amesema hataruhusi mtu yeyote kudharau kazi ya mwengine na kusisitiza kwamba ni lazima wakenya washirikiane katika kuwajibikia majukumu ya taifa hili ili lipige hatua kimaendeleo.
Akizungumza katika chuo cha mafunzo ya makurutu wa polisi cha Embakasi kaunti ya Nairobi wakati wa halfa ya kufuzu kwa maafisa tawala, Rais Ruto amewarai maafisa hao pamoja na wakenya kukumbatia mpango wa upanzi wa miti.
Kwa upande wake Naibu Rais Rigathi Gachagua, amewashauri maafisa wa usalama kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao ya kuimarisha usalama wa taifa huku akiwataka kujitenga na maswala ya siasa.
Naye Waziri wa usalama wa ndani nchini Kithure Kindiki amemuahakikishia rais kwamba idara ya usalama nchini itahakikisha inazingatia kanuni zote za kuimarisha usalama wa nchi bila ya kuegemea upande wowote.
Wakati uo huo Inspekta jenerali wa Polisi nchini Japhet Koome amemuakikishia rais kwamba tayari amefanya mazungumzo na maafisa waliofuzu na kuafikiana kulitumikia taifa hili bila ya ubaguzi, ukabila wala siasa.