Picha kwa hisani –
Naibu Rais Dkt William Ruto amewataka vijana kutokubali kutumiwa na baadhi ya wanasiasa ili kuzuia vurugu na malumbano yanayoshuhudiwa wakati wakenya wanapokaribia uchaguzi mkuu.
Akiwahutubia wakaazi wa eneo la Watamu katika kaunti ya Kilifi wakati wa ziara yake ya siku tatu eneo la Pwani, Ruto amesema matamshi ya chuki na uchochezi kwa vijana huchangia taifa hili kutokuwa na utulivu na amani.
Ruto amesisitiza haja ya wakenya kuungana na kushirikiana katika kuimarisha uchumi wa taifa hili.
Wakati uo huo, amesisitiza kuwa serikali ya Jubilee bado itaendelea kutimiza ahadi iliyotoa kwa wakenya huku akionekana kuukosoa mchakato wa kuifanyia marekebisho katiba wa BBI.
Ruto alikuwa ameandamana na Mbunge wa Malindi Aisha Jumwa, Mbunge wa Kilifi Kaskazini Owen Baya, Mbunge wa Lungalunga Khatib Mwashetani miongoni mwa viongozi wengine.