Story by Our Correspondents –
Naibu Rais Dkt William Ruto amewashauri wakenya kutokubali kushawishiwa na siasa za chuki na ukabila, akisema taifa hili linahitaji mshikamano wa kila mmoja.
Akizungumza katika mikutano yake ya kisiasa katika eneo la Kakamega, Ruto amesema mikakati mwafaka itaidhinishwa ili kuhakikisha vijana na akina mama wanajengwa uwezo wa kibiashara na kuimarisha maisha yao.
Ruto amewataka wanasiasa wanaolenga kuwania viti mbalimbali vya kisiasa kuhakikisha wanatambua maslahi ya wananchi kwanza iwapo kweli wanalenga kubadili uongozi wa taifa hili.
Wakati uo huo amewashauri wananchi kuhakikisha wanazidi kudumisha amani ili taifa hili liendelee kuimarika kiuchumi na maendeleo nchini.