Picha kwa Hisani –
Naibu Rais Dkt William Ruto, ameandaa mkutano wa kupinga zoezi la kukusanya saini kupitia mchakato wa BBI, akisema zoezi hilo linaweza kusubiri hadi mwaka 2022.
Katika mkutano huo ambao umehudhuria na Magavana 7 na wabunge 146 wa bunge la kitaifa na Seneti kule Nairobi, Ruto amesema kuna haja ya maswala ya msingi kujumuishwa katika ripoti ya BBI kabla ya kuandaa Referendum.
Aidha amependeleza fedha zilizotengea kura ya maoni mwaka ujao, zitumika katika kugharamia janga la Corona nchini sawia na kusaidia wanafunzi shuleni pindi shule zitakapofunguliwa Januari mwaka ujao.
Kwa upande wake Gavana wa Turkana Josphat Nanok amesema swala la uwajibikaji katika idara za serikali na pendekezo la Ombudsman katika Mahakama yamekosa kuangaziwa vizuri katika ripoti ya BBI.
Akizungumza katika mkutano huo, Mbunge wa Malindi Aisha Jumwa amependekeza fedha zilizotengewa machakato wa BBI kutumika kukabiliana na janga la Corona, huku akitaka swala la dhulma za kihistoria kanda ya Pwani kuangaziwa kwanza.
Naye mbunge wa Garissa mjini Aden Duale amesema kuna haja ya wakenya kuipinga ripoti ya BBI kwani Referendum itatumia zaidi ya shilingi bilioni 14, akipendekeza BBI kusubiri hadi mwaka 2022.