Story by Our Correspondents –
Naibu Rais Dkt William Ruto ameweka wazi kwamba serikali ina jukumu la kuhakikisha kila kijana anajengwa uwezo wa kujiimarisha kiuchumi kupitia miradi mbalimbali inayozinduliwa na serikali.
Ruto aliyekuwa akizungumza katika kaunti ya Kitui wakati wa mikutano yake ya kisiasa amesema mikakati iliyowekwa tangu serikali ya Jubilee iingie mamlakani haijakamilika kutekelezwa.
Ruto amesema mikakati hiyo ataendelea kutekelezwa iwapo wakenya watamchagua kama rais wa taifa hili wakati wa uchaguzi mkuu ujao, huku akihoji kuwa kuna haja ya vijana na akina mama kusaidiwa kuimarisha uchumi wa nchi.
Ruto hata hivyo amekosoa kutoafikiwa kwa mpango wa ajenda nne kuu ya maendeleo ya serikali ikiwemo afya bora kwa wote, akidai kwamba mpango huo ulishindwa kutekelezwa kutokana na mchakato wa BBI.