Picha kwa hisani –
Naibu wa Rais Dkt William Ruto amesema hakuna tofauti zozote za kiuongozi kati yake na Rais Uhuru Kenyatta na kwamba anatekeleza majukumu yake kutokana na maagizo anayopewa na kiongozi wa taifa.
Akizungumza wakati wa mkutano wa kisiasa katika kaunti ya Isiolo, Ruto amesema licha ya kupokonywa baadhi ya majukumu yake kama naibu wa rais, ataendelea kushirikiana na rais Kenyatta ili kufanikisha ajenda za serikali.
Ruto amesema viongozi wa upinzani waliojiunga na serikali wamesababisha mvutano wa kiuongozi serikalini, akiwataka viongozi hao kurejea katika kambi yao ya upinzani ili kutoa nafasi kwa serikali kufanikisha ajenda za maendeleo.
Kwa upande wake Mbunge wa Malindi Aisha Jumwa aliyekua ameandamana na naibu wa rais kaunti ya Isiolo, amemtaka rais Uhuru Kenyatta kufanikisha ajenda nne kuu za serikali badala ya kuzindua miradi midogo midogo.