Rubani mwanafunzi kutoka taasisi ya Kenya school of Flying amenusurika kifo baada ya gurudumu moja la ndege kuchomoka akiwa angani.
Akithibitisha kisa hicho meneja wa uwanja wa ndege wa Malindi Mohamed Karama amesema kuwa mwanafunzi huyo wa kiume alikuwa anaendelea na mazoezi yake angani kabla ya ndege hiyo aina ya CESNA 152 kukumbwa na hitilafu hiyo.
Karama amesema imemlazimu mwanafunzi huyo kusalia angani mwa mda wa masaa mawili na kufuata mwongozo wa mawasiliano huku asasi mbali mbali za usalama zikipiga kambi katika uwanja huo wa ndege wa Malindi kutafta jinsi ya kumwokoa mwanafunzi huyo.
Aidha Karama amehoji kwamba licha ya kisa hicho cha mapema leo shughuli katika uwanja huo wa ndege wa Malindi zimeendelea kama kawaida.
Hata hivyo mwanafunzi huyo ametua salama bila majeraha na kukimbizwa katika hospitali ya kibinafsi ya Tawfiq kufanyiwa uchunguzi zaidi wa kimatibabu.