Rubani mmoja wa kiume anauguza majeraha makali baada ya ndege yake iliyopaa kutoka uwanja wa ndege wa Malindi, kuanguka katika eneo la Furunzi, kaunti ya Kilifi.
Meneja wa uwanja wa ndege wa Malindi Mohamed Karama amethibitisha kisa hicho akisema kwamba ndege ya rubani huyo iliyokuwa inaelekea uwanja wa ndege wa Ukunda katika kaunti ya Kwale, imeangukia nyumba baada ya kugusa nyaya za umeme.
Karama amesema kwamba rubani huyo alikua amehitimu kuendesha ndege baada ya kufuzu katika chuo cha mafunzo ya urubani cha Kenya School of Flying .
Tayari uchunguzi umeanzishwa kufuatia kisa hicho huku rubani huyo akipelekwa katika hospitali ya kibinafsi ya Tawfiq kwa matibabu.
Taarifa na Charo Banda