Picha kwa hisani
Mwanamuziki maarufu wa mtindo wa R n B’s kutoka Marekani Rihanna ametajwa na jarida la uingereza la ‘The Sunday Times’kama msanii wa Kike tajiri zaidi. Utajiri wake umetajwa kama zaidi ya Paundi milioni 468.
Hii ni mara ya kwanza kwa Rihanna kuingia kama orodha hiyo baada ya kuhamia jijini Londonmwaka jana. Utajiri wake huo umechangiwa na mafanikio makubwa ya kampuni yake ya Fenty Cosmetics na mikataba mingine ya ushirika wa kibiashara pamoja na mapato yake ya sanaa ya muziki.
Rihanna ni ,msanii wa tatu kwenye orodha hiyo ya wasanii tajiri kutoka Uingereza , nyuma ya Paul McCartney na Lloyd Webber ambao wote wana utajiri wa Pauni Millioni 800.
Hii ndio orodha ya wnamuziki matajiri zaidi wa Uingereza.
- Lord Lloyd Webber (£800m, Down £20m)
- Sir Paul Mccartney (£800m, Up £10m)
- Rihanna (£468m, New)
- Sir Elton John (£360m, Up £40m)
- Sir Mick Jagger (£285m, Up £10m)
- Olivia And Dhanni Harrison (£270m, Up £20m)
- Keith Richards (£270m, Up £10m)
- Sir Ringo Starr (£260m, Up £20m)
- Michael Flatley (£206m, Up £2m)
- Ed Shreen (£200m, Up £40m) – Sir Rod Stewart (£200m, Up £10m) – Sting (£200m, No Change)