Shirika la kupambana na utumizi wa dawa za kulevya la ‘Reachout Centre Trust limepokea watumizi 50 wa dawa za kulevya tangu mwanzoni mwa mwaka huu, waliofikishwa mahakamani kabla ya kusajiliwa kwao ili wapokee tiba ya Methadone.
Afisa wa maswala ya haki na afya kwa waraibu katika shirika hilo Suleiman Hassan amefichua kuwa mabadiliko haya katika idara ya mahakama ni mwafaka akisema kuwahukumu na kuwafunga jela waraibu hakuwasaidii kuwanasua kwenye janga hilo.
Hassan amesema ushirikiano kati ya Shirika la Reachout na idara ya mahakama utaimarishwa ili kuwawezesha watumizi wa dawa za kulevya kupata haki, matibabu na kuwezeshwa kujikimu kimaisha.
Taarifa na Gabriel Mwaganjoni