Shirika la ‘Reachout Center Trust’ limeanzisha mradi wa kuwanasua wavutaji shisha kutoka kwa uraibu huo.
Mkurugenzi mkuu wa shirika hilo Taib Abdhulrahman amesema vijana wengi katika kaunti ya Mombasa wameathirika na uvutaji shisha kutokana na tabia ya kuiga mienendo ya watu wa mataifa ya nje.
Taiba amesema wadau wa kupambana na utumizi wa mihadarati nchini wanafaa kuzidisha hamasa kwa vijana wa Mombasa kuhusu athari za utumizi wa dawa za kulevya.
Wakati uo huo ameitaka jamii kushirikiana na mashirika ya kupambana na mihadarati ili kuona kwamba vita dhidi ya dawa za kulevya vinafaulu.
Taarifa na Hussein Mdune.