Kufuatia ukosefu wa vituo vya kuwarekebishia tabia waraibu wa kike wa dawa za kulevya hapa Pwani ,sasa shirika ‘Reachout Center Trust’ limepanga kuwafikia Wanawake hao mashinani na kuwanasua.
Mkurugenzi mkuu wa Shirika hilo Taib Abdulrahman amesema kwamba idadi ya wanawake wanaotumia dawa za kulevya inazidi kuongezeka.
Taib hata hivyo amefichua kwamba miradi inayowalenga Wanawake inayoendelezwa na shirika hilo imebadilisha maisha ya watumizi hao.
Amesema mradi wa kuwafundisha waraibu hao kazi za ususi uliyozinduliwa hivi majuzi tayari umepelekea waraibu wa kike kuwa na ari ya kujifunza taaluma hiyo ili waidhinishe miradi yao ya kiuchumi na kukabiliana na uhaba wa ajira.
Taarifa na Gabriel Mwaganjoni.