Jumla ya timu 32 za Mpira wa vikapu katika kaunti ya Mombasa zinashiriki michuano ya simu mbili ya Mpira wa vikapu katika ukumbi wa KPA eneo la Makande Kaunti ya Mombasa.
Michuano hiyo inajumuisha timu za Mpira wa vikapu za wanaume na akina Dada.
Kulingana na waandalizi wa michuano hiyo ambalo ni Shirika la kupambana na uraibu wa dawa za kulevya nchini la Reachout Centre Trust, kutokana na changamoto ya uraibu wa dawa za kulevya katika Kaunti hiyo ni vyema iwapo vijana wataletwa pamoja na kusaidiwa kukuza talanta zao ili wazitumie vilivyo katika kujikimu kimaisha mbeleni.
Mkurugenzi mkuu wa Shirika hilo Taib amesema kwamba mbali na kuwahusisha vijana katika Spoti ili kuwakinga na athari za uraibu wa dawa za kulevya vile vile michuano hiyo inatumika kuwarai vijana kukumbatia spoti na kuitumia vilivyo katika kujipatia mapato.
Michuano hiyo ni ya pili baada ya Shirika hilo la Reachout kuzindue kipute cha soka cha ‘Pamba roho’ kinachoendelea katika Kaunti ya Mombasa ambacho vile vile kina malengo ya kuwakinga na kuwaelimisha vijana kuhusiana na athari za Mihadarati na maambukizi ya virusi vinavyochangia ukimwi.
Taarifa na Gabriel Mwaganjoni.