Picha Kwa Hisani –
Mwanamuziki mkongwe wa Bongo Fleva Ray C ametoa ushauri wake kwa wanamuziki Harmonize na Rayvanny ambao wanaendelea kuvuana nguo kwenye mitandao.
Wamiliki hao wa kampuni za Konde Music na Next Level Music mtawalia kwa siku za hivi karibuni wamekuwa wakiaibishana kwenye mitandao kuhusu visa vya mapenzi vinavyohusu mama na mtoto Frida Kajala na Paula Kajala.
Rehema Chalamila ambaye sikuhizi anaishi Ufaransa kupitia akaunti yake ya Instagram alipacika video ya mwanamuziki wa Nigeria Burna Boy ambaye alishinda tuzo la Grammy na chini yake akaandika maneno yafuatayo;
“Tunawakubali kinyama!! sema mnatuletea Pwagu na Pwaguzi Taarabu……Na nyie ni watoto wa kiume halafu mko juu vibayavibaya….Sasa!!!.Wakati mnapoteza muda kushushana na kuaibishana wenzenu wanabebana mpaka kwenye magrammy!!!Ukumbi mshaachiwa sasa msituzingue na nyie….Afu kumbukeni hii ni insta. Na mna mashabiki nje ya bongo wanaowafuatilia. Msidhani hawaoni huu upupu wenu Wanaona yote na hao wasanii wa nchi jirani 🇳🇬ambao ndo mnaopambana nao kufika walipo nao wanayaona afu wanawachora KINYAMAA!Hapa ni Instagram, Sio Bongo!So mnachoposti na kinachotrend kinaonekana kote. Kwakweli mnajichoresha..Yani kwa kifupi NI NOMA.Hata kama ni mashindano sio kwa style hii mnazoleta na kiki zenu za ajabu ajabu……Hata hamfananii…MNAZINGUA KINOMA…Acheni hizo ingieni studio muendelee kutuwakilisha vile mlivyotuzoesha.Haya mnayofanya sasa ni ya kibwege sana afu YAKISHAMBA..
FOCUS……acheni hizo.Na mkilewa sifa za kibwege kama hizi mnakoelekea mtakuja kuwekeana hadi sumu mmalizane….Mkataeni huyo pepo mana kashawaingia!”
Ray C wa umri wa miaka 38 sasa, hajatoa kazi mpya ya muziki kwa muda sasa.