Shirika la huduma za Feri limetangaza kufanya mipangilio mipya ya huduma zake ili kuhakikisha watumizi wa kivuko cha Likoni wanahudumiwa vyema.
Mwenyekiti wa bodi ya usimamizi wa shirika hilo, Dan Mwazo amesema kuwa wanapania kuboresha huduma hizo ikiwemo kuweka magari maalum ya watu wanaoishi na ulemavu, kukaguliwa kwa magari na wasafiri kupitia njia mpya za kijiditali sambamba na kuhakikisha kuwa feri zinazotumika katika kivuko hicho zinachukua mda mchache kama ilivyo kwa sasa.
Mwenyekiti huyo amesema kuwa serikali kupitia shirika hilo inapania kupanua eneo la kivuko hicho ili kuhakikisha kuwa msongamano wa watu pamoja na magari inathibitiwa.
Mwazo amabye alikua ameandamana na mkurugenzi wa shirika la Feri Bakari Hamisi pamoja na wanachama wengine wa bodi hiyo amesema kuwa kama shirika wanalenga kusambaza huduma hizo katika maeno ya ziwa Victoria na maeneo ya Lamu ili kurahisisha usafiri kwa wakazi katika maeneo yenye kuzungukwa na maji nchini.