Picha kwa Hisani –
Seneta wa kaunti ya Taita taveta Jones Mwaruma ameitaka serika ya kitaifa kutekeleza sheria ya mwaka 2016 ya kuhakikisha wananchi wananufaika na raslimali zilizoko katika maeneo yao.
Mwaruma amesema sheria hiyo imeweka wazi kuwa wananchi anafaa kupata asilimia 5 ya mapato yanayotokana na uchimbaji madini, sheria ambayo haijatekelezwa hadi sasa.
Akizungumza katika kaunti hiyo, Mwaruma ameitaka Wizara ya Utalii nchini kuhakikisha kaunti ya Taita taveta inanufaika na mapato yanayotokana na mbuga za Wanyama pori za Tsavo.