Tetesi ambazo zimekuwa zikienea kwa miezi sasa kuhusu mwanamuziki wa kizazi kipya Jaffaryzo, anyejulikana kwa wimbo wake maarufu ‘Piga U Turn’, kutoka kwa recording label ya ATL Music, zimethibitishwa na rafiki yake wa karibu ambaye ni rapper Rama K. Rama K ambaye amemshirikisha mwanamuziki huyo kwenye ngoma yake mpya inayoitwa ‘Taharifa’ ameeleza sababu ya mwandani wake kutoka katika recording label hiyo.
Kupitia mahojiano ya simu katika kipindi cha Kaya Flavaz, Rama amekiri kuelezewa kilicho msibu Jaffaryzo na kumpelekea kutoka ATL Music. Jaffaryzo pia alimpa ruhusa ya kuimba matukio hayo kwa ngoma hiyo ‘Taharifa’. Rama alifafanua maana ya mistari hii mwanzoni mwa ngoma hiyo, “… mahaba yenye hali yamemkaba shir asilimia kwenye koo…” na kusema kwamba Producer Shirko wa Shirko media alimpendelea sana msanii mmoja wa ATL, ambaye ni Ally Mahaba na kuwasahau wasanii wengine, sababu iliyompelekea Jaffaryzo kutoka ATL.
Hata hivyo, Producer Shirko aliweka wazi kuwa mwanamuziki huyo hakuwa na nidhamu na hivyo basi kutolewa kwa recording label hiyo na meneja wake Ambrose Lewa. Kama tu alivyoelezea Ally, producer huyo pia alisema bidii ya Ally Mahaba ya kuandika nyimbo mara kwa mara na kumueleza meneja wake ndio inayosababisha malalamishi hayo. Shirko pia aliweka wazi kumwandikia Jaffaryzo wimbo huo wa ‘Piga U turn’ uliyofanya vizuri sana ndani na nje ya mkoa wa Pwani.
“ATL na Shirko media ni vitu tofauti, isipokuwa mimi ndio kama official producer wa, kuwa wanapokuwa tayari kufanya kazi yoyote , wanakuja hapa wanalipa hela, wanakuja kufanya kazi. Kwa hiyo sasa Ally alikuwa anapenda kukaa na boss wake anamwambia ana kazi angependa kufanya, kisha boss wake anasikiliza idea akipenda ananipigia kuniambia kesho Ally anakuja… Jaffaryzo naye tulikuwa tunampush sana kumwambia ana ngoma moja na ina muda sasa, fanya kazi na nilikuwa namwandikia ngoma mimi, kitu ambacho sikutaka kukisema… Na yeye kutoka ATL ni swala la nidhamu, Jaffaryzo anajitetea kwa marafiki zake tu lakini ukweli ni kwamba alitolewa ATL kwa sababu ya nidhamu na alivumiliwa sana na boss wake pamoja na kuwa alikuwa anasaidiwa…” – Producer Shirko.
Aidha Ally alisema hana bifu yoyote ile na Jaffaryzo na kumuita kakake na kuwa anamtambua kimuziki kwani alimtangulia kwenye industry.
Je, unalizumziaje swala hili?