Picha kwa hisani –
Story by Correspondents-
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amepokea chanjo ya Corona ya Johnson na Johnson baada ya kuzindua rasmi zoezi la kuwachanja wananchi wa Tanzania chanjo hiyo ili kuzuia maambukizi ya virusi vya Corona.
Akilihutubia taifa la Tanzania katika halfa hiyo ilioandaliwa katika Ikulu ya Dar-es Salam, Rais Samia amesema japo zoezi hilo ni la hiari, chanjo hiyo ina uwezo mkubwa wa kuzuia msambao wa virusi vya Corona.
Rais Samia amesema japo serikali ya Tanzania imepokea dozi milioni moja pekee na idadi ya watanzania ni kubwa, kuna haya watanzania kuchukua tahadhari katika kupambana na maambukizi ya Corona.
Kwa upande wake Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa amejitokeza kupokea chanjo hiyo huku akiweka wazi kwamba serikali ya taifa hilo haina dhamira yoyote mbaya kwa wananchi wake katika mpango wa kuwachanja chanjo ya Corona.
Hatua hiyo ya serikali ya Tanzania imejiri baada ya utawala wa Hayati John Pombe Magufuli kupinga chanjo za Corona huku ikisisitiza kwamba virusi hivyo vinaweza kutibiwa kiasili, mtizamo ambao umebadilishwa na utawala wa rais Samia.