Mmoja wa watu wa familia tajiri zaidi za kifalme duniani Rais wa milki za kiarabu (UAE) Sheikh Khalifa bin Zayed al-Nahyan amefariki akiwa na umri wa miaka 73.
Sheikh Khalifa alikuwa rais wa milki za kiarabu (UAE) tangu mwaka 2004 lakini wadhfa wake kwa kiasi kikubwa haukuwa na mamlaka tangu alipopata maradhi ya kiharusi mwaka 2014.
Kaka yake, Mohamed bin Zayed al-Nahyan, sasa ndiye anayeongoza masuala ya kitaifa.
Rais wa UAE, Sheikh Khalifa alikuwa mtawala wa Abu Dhabi mji mkuu wenye utajiri wa mafuta wa milki saba zinazounda Muungano wa nchi za kiarabu
Taarifa ya kifo chake imetangazwa na serikali ya taifa hilo huku Wizara ya masuala ya rais ikitangaza siku 40 za maombolezo na kuperurushwa kwa bendera nusu mlingoti kuanzia na shughuli za kazi zikihairishwa katika sekta za umma na kibinafsikwa muda wa siku tatu.