Picha kwa hisani –
Rais wa Ethiopia,Sahle-Work Zewde ametembelea Tanzania, katika ziara ya siku moja.
Waziri wa Mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof Palamagamba Kabudi awali alisema Mkuu huyo wa taifa la Ethiopia atafika na salamu mahususi kwa Rais wa Tanzania lakini pia kuongelea masuala ya uhusiano kati ya Tanzania na Ethiopia.
Rais Work Zewde amewasili mjini Chato asubuhi hii na kupokelewa na Mwenyeji wake Rais wa Tanzania, John Magufuli.