Rais wa taifa la Chad Idriss Deby amefariki dunia.
Taarifa hiyo imetangazwa na jeshi la taifa hilo kwamba Mwendazake amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 68 baada ya kupata majeraha kwenye mapambano dhidi ya waasi.
Mapambano hayo yamechochewa na waasi ambao waliingia nchini humo kutokana taifa la Libya.
Idriss amefariki dunia siku chache tu tangu matokeo ya awali ya uchaguzi wa urais kufanyika nchini humo mwezi Aprili 11 na kuonesha kuwa anaongoza kwa asilimia 80.
Kwa sasa Serikali ya Chad na bunge limevunjwa na baraza la kijeshi nchini humo likishikilia uongozi wa taifa hilo kwa kipindi cha miezi 18 ijayo chini ya uongozi wa mwanawe idriss, Mahamat Deby.