Picha kwa hisani –
Katika kile kinachoonekana kama ‘ishara njema’ katika kutatua mzozo wa kidiplomasia kati ya Rwanda na Burundi, Rais wa Burundi Evariste Ndayishimiye amesema anaamini nchi hizo mbili zitakuwa tena na uhusiano mwema hivi karibuni.
Uhusiano wa Burundi na Rwanda uliingia dosari tangu mwaka 2015, baada ya kila upande kuushutumu mwingine kuunga mkono mashambulio dhidi ya mwingine.
Akizungumza na wanahabari Rais Ndayishimiye amesema utatanishi wa viongozi wa nchi hizo mbili unaonekana na pia”sababu ya mzozo inafahamika na kwamba ana imani mataifa hayo yatakua na mapatano.
Viongozi wa Burundi wanawashutumu viongozi wa Rwanda kwa kuwapa hifadhi baadhi ya watu waliojaribu kuupindua utawala wa Burundi mwaka 2015, shutuma ambazo Rwanda inazikanusha.