Story by Our Correspondents-
Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa amewasili humu nchini kwa ziara ya siku mbili ya kiserikali.
Rais huyo wa Afrika kusini amepokelewa na mwenyeji wake Rais William Ruto na kupewa heshima ya kitaifa kwa kupigiwa mzinga 21 sawa na kulikagua gwaredi za jeshi la ulinzi nchini.
Rais Ramaphosa na mwenyeji wake Rais Ruto kwa sasa wako katika kikao cha faraja kujadili kuhusu maswala mbalimbali ya kimataifa ambapo swala la uhusiano mwema wa kibiashara, usalama, uwekezaji na maswala mengine kati ya mataifa hayo mawili yatawekwa wazi.
Hata hivyo swala la kongamano la biashara linatarajiwa kuandaliwa humu nchini pia ni kati ya ajenda zilizopewa kipau mbele sawa na mikataba ya kulegezwa Visa ya usafari kwa wakenya wanaolenga kufanya biashara nchini Afrika kusini.